Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

Maadhimisho ya Miaka 50 ya TET

Profile ya TET

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ni Taasisi ya umma iliyo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. TET ilianzishwa rasmi mwaka 1975 kwa Sheria ya Bunge Na. 13 ya Mwaka 1975. TET ina mamlaka ya kutekeleza majukumu yafuatayo:

  1. Kubuni, kuandaa na kuboresha Mitaala ya Ngazi za Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu pamoja na kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Mitaala.
  2. Kuandaa vifaa saidizi vya kutekeleza mitaala na kutathmini ubora wa vifaa vinavyolengwa kutumiwa katika Ngazi za Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu
  3. Kutoa mafunzo kwa watekelezaji na wasimamizi wa mitaala ili waweze kutekeleza mitaala kwa ufanisi.
  4. Kufanya tafiti za kielimu na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali na wadau wa elimu katika masuala ya mitaala, ufundishaji na ujifunzaji na ubora wa elimu nchini.

Dhima

Kuwa kitovu cha ubora katika ubunifu, uandaaji, ukuzaji na utekelezaji wa mitaala kwa kutumia wataalamu wenye ari na uwezo wa hali ya juu katika fani zao.

 

Dira

Kuwezesha mchakato wa utoaji elimu bora kupitia mitaala bora ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu

 

Mafanikio ya TET

  1. Kuandaa mitaala bora inayokidhi mahitaji ya jamii na matarajio ya serikali.
  2. Kuandaa, kuchapa na kusambaza vitabu vya kiada kwa uwiano wa 1:3.Kutafsiri, kuchapa na kusambaza vitabu vya maandishi makubwa na Breli kwa uwiano wa 1:1.
  3. Kuandaa maktaba mtandao inayosambaza machapisho ya TET.
  4. Kuandaa kamusi ya alama kwa ajili ya wanafunzi wenye uziwi.
  5. Kuanzisha TET Soma Kwanza TV ambayo imelenga kuandaa na kurusha maudhui ya kielimu ikiwemo vipindi mbalimbali katika mtaala.
  6. Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji
  7. Kuandaa mfumo maalumu ambao umepakiwa maudhui ya kieletroniki kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
  8. Kuongeza hazina ya vitabu vya rejea, riwaya, hadithi, ushairi na aina nyingine za uandishi bunifu.
  9. Kuongeza uchapaji na usambazaji wa machapisho  ya TET.
  10. Kuongeza idadi ya wafumishi wenye weledi na uzoefu wa kitaaluma na kitaalamu.

 

Katika kutimiza majukumu yake, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Mwaka huu 2025 inafanya maadhimisho ya Miaka 50 tangia kuanzishwa kwake, huku tayari shughuli mbalimbali zikitekelezwa.

 

Shughuli Mbalimbali/Matukio yaliyofanyika kuelekea Miaka 50 ya TET

  1. Uzinduzi wa usambazaji wa vitabu bunifu vilivyoshinda tuzo ya Mwl. Nyerere. (18 Novemba, 2024- Waziri wa Elimu)
  2. Utangazaji wa kazi za TET kwa umma(Desemba, 2024 – Juni, 2025, Media za utangazaji (Mitandao ya kijamii, Magazeti, Vituo vya TV na Redio)
  3. Utoaji wa mafunzo ya mtaala ulioboreshwa kwa walimu wa shule za sekondari za umma na binafsi kwa njia ya ana kwa ana na Darasa Janja katika Halmashauri zote. (Desemba, 2024-Juni, 2025 - Wakuza Mitaala, Viongozi na wakufunzi)
  4. Matembezi ya hisani na uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya TET. (07 Machi, 2025,Yataanzia Ofisi za TET Mikocheni cha Dar-es-Salaam na kumalizikia Ofisi za TET - Mgeni rasmi Waziri Mkuu, Mhe. Kassimu M. Majaliwa (Mb) • Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia)
  5. Uzinduzi na kukabidhi maabara ya TEHAMA Wilayani Lushoto. (15 Machi, 2025 - Shule ya Msingi Shukilahi • Shule ya Sekondari Magamba, Baraza na Menejimenti ya TET)
  6. Kutengeza makala kuhusu TET kwa kuwahoji wakurugenzi wakuu waliowahi kuongoza TET pamoja na wadau wa TET zikiwemo shule za umma na binafsi. (01 Jan – 16 Machi, 2025 TET Makao Makuu na mahali walipo viongozi husika, Ofisi ya PRO • Wakurugenzi wastaafu)
  7. Uchapaji kitabu cha historia ya miaka 50 ya TET. (30 Machi, 2025- Kamati ya uandishi • Wastaafu wa TET • Wahariri • Msanifu • Mchapishaji)
  8. Uendeshaji wa mafunzo ya ushauri na unasihi kwa wakuza mtaala na walimu(Machi Juni 2025 - Chuo Kikuu cha Agha Khan • Wakuza Mitaala • Walimu)
  9. Upandaji wa miti (Msitu bustani)(01 Aprili, 2025 - Wafanyakazi - TET • Agha Khan Foundation • Wanafunzi • Viongozi wa elimu na walimu • Wadau wa maendeleo • Wanahabari)
  10. Kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya TET. (27 Juni, 2025 - Mgeni rasmi (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) • Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia • Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia • Viongozi wa Serikali • Wadau wa elimu).

 

Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania