Muundo wa TET
Muundo wa taasisi hutumika kuiwezesha TET kusimamia dira na majukumu yake ya msingi. Juu kabisa ya muundo wa TET lipo Baraza lenye wajibu wa uongozi kisheria na huwajibika kwa Waziri mwenye dhamana ya elimu. Chini ya Baraza hilo yupo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi mwenye mamlaka ya utendaji wa kazi za taaluma na uendeshaji.
Kulingana na Muundo wa mwaka 2009, chini ya Mkurugenzi Mkuu zipo idara nne za taaluma na vitengo tisa vya uendeshaji ambavyo kwa pamoja huiwezesha TET kutekeleza majukumu yake ya msingi kama yalivyo katika Sheria Na. 13 ya mwaka 1975 iliyoanzisha taasisi.
Idara za taaluma ni Ukuzaji na Uboreshaji wa Mitaala; Ubunifu na Utayarishaji wa Vifaa vya Elimu; Utafiti, Habari na Machapisho na Kituo cha Mafunzo ya Mitaala. Vitengo vya uendeshaji ni Rasilimali Watu na Utawala; Fedha; Ukaguzi wa ndani; Sheria; Ugavi na Manunuzi; Uchapaji; Mipango; Teknlojia ya Habri na Mawasiliano; na Uhusiano na Masoko.
Soma zaidi kuhusu Muundo wa TET wa Mwaka 2009
TET inaendelea na kazi ya kukamilisha kazi ya kuboresha muundo wake wa mwaka 2009.