TET KUSHRIKIANA NA TAASISI YA US PEACE CORPS KATIKA KUBORESHA ELIMU
Imewekwa: 26th May, 2022
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imekubali
kufanya ushirikiano na Taasisi ya US PEACE CORPS ya nchini Tanzania
inayojihusisha na huduma za kujitolea za Wamarekani katika kuboresha
eneo la ujifunzaji na ufundishaji hapa nchini.
Taasisi hiyo ya US PEACE CORPS
huleta walimu wa kujitolea nchini kutoka nchini Marekani ambao hufanya
kazi za kufundisha katika shule mbalimbali nchini watakazopangiwa walimu hao.
Katika kikao cha mazungumzo
kilichomuhusisha Mkurugenzi mwakilishi nchi wa shirika la US PEACE wa
shirika hilo Bi.Stephanie Joseph na Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth
Komba na wadau wengine wa taasisi hizo, wamekubaliana kuwa na ushirikiano
na kubadilishana uzoefu katika kupitia moduli za kufundishia walimu hao
wanaojitolea ili ziendane na tamaduni za Kitanzania.
Dkt.Aneth Komba amesema kuwa TET ipo tayari
kufanya kazi na taasisi hiyo inayojitolea nchini Tanzania kuimarisha ujifunzaji
wa masomo ya Sayansi.
“Tutabadilishana nao uzoefu katika maeneo
mbalimbali na hasa eneo la mitaala na kupitia moduli zao za ufundishaji
ziweze kuendana na utamaduni wetu” amesema Dkt.Komba.