TET yawasilisha bungeni maoni ya wadau kuhusu uboreshwaji wa mitaala ya elimu
Imewekwa: 08th November, 2021
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imewasilisha maoni ya wadau kuhusu uboreshaji wa Mitaala kwa Ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma Novemba 8, 2021.
Katika wasilisho hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth
Komba amewaeleza wajumbe wa kamati hiyo namna TET ilivyofanikiwa kupata
maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya uboreshaji wa Mitaala.
Amesema TET imepokea maoni yenye maudhui mbalimbali
ambayo watalaamu wa TET wanaendelea kuyachambua kwa ajili ya kuboresha Mitaala
iliyopo.
Vilevile, Dkt. Komba ameieleza kamati hiyo kuwa
ukusanyaji wa maoni ulioanza mwaka huu unatarajiwa kukamilika Juni, 2022.