Kongamano la Kitaifa la Elimu laanza jijini Dodoma
Imewekwa: 12th May, 2023
Kongamano la Kitaifa la Wadau wa Elimu nchini kuhusu uhuishaji wa Sera na Mitaala ya Elimu limeanza leo tarehe 12-14/05/2023 katika ukumbi wa Jakaya Convetion Center jijini Dodoma ambapo wadau mbalimbali wameshiriki wakiongozwa na Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda aliyemuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Katika kongamano hilo Mhe, Mkenda amewaambia wadau wa Elimu nchini kuwa ni nafasi yao kutoa maoni yatakayotumika katika marekebisho ya Rasimu ya Sera na Mitaala ambapo utekelezaji wake utaanza mwakani 2024.
Wageni mbalimbali wameshiriki katika kongamano hilo akiwemo Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ,Mhe. Rosemary Senyamule,Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Tekonolojia Prof.Carolyine Nombo , Naibu Katibu Mkuu Sayansi Prof. James Mdoe na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo ,Prof.Kitila Mkumbo na wajumbe wa kamati hiyo.
Vile vile ,wageni wengine ni wenyeviti wa kamati za sera na Mitaaala pamoja na wajumbe wote ,Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Prof. Maulid Mwatawala Tanzania wajumbe wa Baraza, Mkrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Dkt. Aneth Komba na wajumbe wa menejimenti.