Tangazo la Mafunzo kabilishi kwa Walimu kuhusu Mtaala ulioboreshwa
Imewekwa: 23rd August, 2019
Mafunzo kabilishi kwa Walimu kuhusu Mtaala
ulioboreshwa
Taasisi
ya Elimu Tanzania imeandaa mafunzo kwa walimu wa shule zisizo za serikali
kuhusu Mtaala wa Elimu ya Awali na Msingi Darasa la I-IV ulioboreshwa. Gharama
za mafunzo ni sh. 150,000/= kwa
mwalimu wa Elimu ya Awali na sh
200,000/= kwa mwalimu wa Elimu ya Msingi Darasa la I-IV.
Mafunzo
haya yanatarajiwa kufanyika kuanzia mwezi Septemba, 2019. Taarifa kuhusu eneo
na tarehe kamili ya mafunzo mtajulishwa.
Kwa
shule ambazo hazitajtuma maombi mnaombwa kufanya hivyo kwa kutumia mwongozo
uliooneshwa hapa chini. Malipo yatafanyika baada ya TET kupata taarifa hizi.
Jina la shule
|
Wilaya na
Mkoa
|
Idadi
|
Jina la mwalimu wa Elimu ya Awali
|
Jina la mwalimu
Drs I-II
|
Jina la mwalimu
Drs III-IV
|
Barua pepe
|
Simu
|
Tutashukuru
iwapo tutapata maombi hayo mapema ili tuendelee na maandalizi.
Maombi yatumwe kupitia anuani ifuatayo:
Mkurugenzi Mkuu
Taasisi ya Elimu Tanzania
S. L. P. 35094, DAR ES SALAAM
Barua pepe: director.general@tie.go.tz,
fransisca.tarimo@tie.go.tz
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 6/9/2019
KARIBUNI SANA..