TET na Ofisi ya Elimu ya Gwangju Metropolitan ya nchini Korea Kusini kundeleza ushirikiano wa kitaaluma.
Imewekwa: 12th October, 2023
Tarehe 10/10/2023, Mkurugenzi wa Utafiti, Habari na Machapisho Bwana Kwangu Zabrone ameongoza ujumbe kutoka Ofisi ya Elimu ya Gwangju Metropolitan ya nchini Korea Kusini kutembelea Shule ya Msingi Tegeta 'A' na ya Sekondari Kimbiji.
Shule hizo zinashiriki katika utekelezaji wa mradi wa Korea e-Learning Improvement Cooperation (KLIC) wenye lengo la kuwajengea uwezo walimu kutumia TEHAMA katika mchakato wa ujifunzaji na ufundishaji shuleni .
TET na Gwangju Metropolitan ya Korea Kusini zinatekeleza mradi huo kwa kuwajengea uwezo walimu wa kutumia TEHAMA katika utekezaji wa mtaala kupitia mafunzo pamoja na kugawa vifaa vya TEHAMA katika shule husika ambazo zinatekeleza mradi huo.
Bwana Zabron alieleza kuwa kupitia mradi wa KLIC walimu na wanafunzi nchini wajengewa uwezo wa kutumia TEHAMA katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji.
Ujumbe huo utakuwepo nchini kwa muda wa siku tatu kwa ajili ya kufanya maadalizi ya kuwapokea wanafunzi 27 pamoja na walimu 5 kutoka Korea Kusini watakaowasili nchini mwezi Novemba ambapo wa wanaotarajiwa kuwa nchini mwezi Novemba, 2023 kwa madhumuni ya kuendeleza ushirikiano wa kitaaluma.