Mkutano wa wadau wa elimu kuhusu uboreshaji wa Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari
Imewekwa: 25th June, 2021
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imeandaa mkutano wa wadau wa elimu utakaofanyika Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC) siku ya tarehe 26/06/2021 kuanzia saa 2:00 asubuhi. Mgeni rasmi katika tukio hilo atakuwa Mh. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako (Mb).
Lengo la mkutano huo ni kupokea maoni kutoka kwa wadau wa elimu nchini kuhusu uboreshwaji wa Mitaala ya elimu katika ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari. Wadau wote wa elimu nchini wanakaribishwa kuja kushiriki katika mkutano huo.
Unaweza pia kutoa maoni yako kwa njia ya mtandao kwa kufungua na kujaza fomu iliyopo kupitia kiungnaishi hiki: https://forms.gle/V3pBrYNAn46WnxCb6